THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINING COMMISSION

PROFESA MANYA ATEMBELEA MABANDA YA WIZARA YA MADINI KWENYE MAONESHO YA MADINI GEITA


news title here
27
Sep
2020

Leo tarehe 27 Septemba, 2020 Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini, Profesa Shukrani Manya ametembelea mabanda ya Wizara ya Madini kwenye Maonesho ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayoendelea katika Uwanja wa Kituo cha Uwekezaji Bombambili Geita Majini.

Mara baada ya kutembelea Banda la Tume ya Madini kwenye maonesho hayo amepongeza kazi nzuri iliyofanywa na wataalam wa Tume na kuwataka kuendelea kuelimisha ummahasa wachimbaji wadogo kuhusu Sheria ya Madini na kanuni zake, usalama wa afya na mazingira wanapoendesha shughuli za uchimbaji wa madini na biashara ya madini.

Aidha ameelekeza elimu kuhusu ushirikishwaji wa watanzania kwenye Sekta ya Madini kuendelea kutolewa ili kutoa fursa kwa wananchi wengi kushiriki kwenye sekta ya Madini.