THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINING COMMISSION

DKT. BITEKO ATAKA WATUMISHI MADINI KUFIKIA MALENGO MAKUBWA YA SERIKALI


news title here
13
Mar
2023

Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko amesema Wizara inayo majukumumakubwa iliyopewa na Serikali ikiwemo kuhakikisha Sekta ya Madini inachangia asilimia 10 katika Pato la Taifa ifikapo mwaka 2025.

Ametaka kazi kuwa kipimo cha ukaribu cha utendaji wa kazikwa watumishi wa wizara na taasisi katika kufikia malengo hayo na kuongeza kwamba, Wizara itaendelea kuweka mazingira bora ya kazi kwa watumishi pamoja na taasisi zilizopo chini yake ili kukuza mchango wa Sekta ya Madini kwenye Pato la Taifa.

Dkt. Biteko aliyasema hayo mapema Machi 10, 2023 kwenye kikao chake na watendaji wa Wizara na Tasisi zake kilichofanyika jijini Dodomawakati akimkaribisha na kumtambulisha Katibu Mkuu mpya wa Wizara hiyo, Kheri Mahimbali aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo.

“Kama Wizara tutaendelea kuweka mikakati ya kuhakikisha Sekta ya Madini inaendelea kukua na mchango wake kwenye Pato la Taifa unafikia asilimia 10 ifikapo mwaka 2025 pamoja na uboreshaji wa mazingira ya kazi kwa watumishi wetu pamoja na taasisi tunazozisimamia ili kutoa ari ya kuchapa kazi kwa ubunifu na hata kuvutia watumishi wengine kufanya kazi katika Sekta ya Madini,”alisema Waziri Biteko.

Katika hatua nyingine, alimpongeza Katibu Mkuu mpya wa Wizara Mahimbali kwa uteuzi wake na kuongeza kuwa, Wizara na Taasisi zake itaendelea kumpa ushirikiano wa kutosha lengo likiwa ni kuifanya Sekta ya Madini kuwa miongozi mwa sekta zinazochochea uchumi wa nchi.

Naye, Katibu Mkuu Mpya Wizara ya Madini Kheri Mahimbali akizungumza katika kikao chicho aliwataka wataalam wa Wizara kuweka msukumo kwenye madini ya Kimkakati kutokana na umuhimu wa madini hayo katika kuyafungamanisha na sekta nyingine za kiuchumi.

Alipongeza uongozi na watendaji wa Wizara na taasisi zake kwa kuiwezesha sekta ya Madini kufikia asilimia 9.7 ya mchango wake katika Pato la Taifa na kuwataka kuhakikisha asilimia 0.3 iliyobaki inafikiwa na kuongeza, ‘’tumeletwa hapa kuongeza nguvu, sikuja kumwondoa yoyote kwenye nafasi yake, bado tuna kazi mbele yetu na ninaamini katika kushirikiana,’’.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo aliwataka watumishi wa Wizara ya Madini kutambua dhamana kubwa waliyonayo na matarajio waliyonayo watanzania kupitia rasilimali madini na hivyo kuwataka watumishi kuhakikisha rasilimali madini zinachochea uchumi wa nchi, ukuaji wa sekta nyingine na maendeleo ya watu.

Awali, watendaji kutoka taasisi zilizo chini ya Wizara wakiwasilisha taarifa za utekelezajiwa majukumu yaokatika kikao hicho, sambamba na kupongeza uteuzi wa Mahimbali walieleza mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya madini.

Akizungumzia mafanikio ya Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Kaimu Mtendaji Mkuu Notka Banteze alisema hadi sasa GST imefanikiwa kufanya tafiti za jiolojia kwa asilimia 97 nchi nzima, jeokemia asilimia 24 high density, asilimia 84 low density nageophysics asilimia 16.

Akizungumzia mafanikio ya Tume ya Madini tangu kuanza kwa utekelezaji wa majukumu yake mapema Aprili 2018, Katibu Mtendaji wake Mhandisi Yahya Samamba alieleza kuwa Tume imefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 2.54 ikiwa ni sawa ya asilimia 91.43 ya lengo la kukusanya kiasi cha shilingi trilioni 2.77, uanzishwaji wa masoko ya madini 42 na vituo vya ununuzi wa madini nchini 93.

Aidha, Mhandisi Samamba aliongeza mafanikio mengine kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa thamani ya madini yaliyouzwa nje ya nchi kutoka kilogramu 53,173.39 yenye thamani ya shilingi trilioni 3.547 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019 hadi kilogramu 60,184.8 yenye thamani ya shilingi trilioni 7.336 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 na kupungua kwa ajali kwenye shughuli za uchimbaji wa madini.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Uhamasishaji wa Uwazi na Uwajibikaji katikaRasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI), Miriam Mgaya aliongeza mafanikio yaliyopatikana kuwa ni pamoja na kuongezeka kwa uwazi na uwajibikaji katika mapato yatokanayo na rasilimali za mafuta, madini na gesi asilia na kusisitiza kuwa mpaka sasa TEITI imechapisha ripoti 12.

Naye, Kaimu Mratibu wa Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) Daniel Kidesheni aliishukuru Wizara kwa kukiwezesha kituo hicho kupata fedha kwa ajili ya utekelezaji miradi ambayo itakisaidia kituo hicho kupiga hatua kubwa katika sekta ndogo ya uongezaji thamani madini.