THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINING COMMISSION

TUME YA MADINI YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA KWENYE MAONESHO YA SABASABA


news title here
14
Jul
2020

Tarehe 13 Julai, 2020 Tume ya Madini ilikabidhiwa tuzo ya ushindi mara baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwenye Kundi la Nishati na Madini katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yaliyofanyika katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam

Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo, Katibu Mtendaji wa Tumeya Madini, Profesa Shukrani Manya alisema kuwa siri ya mafanikio ni pamoja na washiriki kutoka Tume ya Madini, Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini na Wadau wa Madini kujituma kwenyeuelimishaji kwa kutumia ubunifu wa hali ya juu wananchi mbalimbali waliokuwa wanatembelea maonesho hayo

Akielezea mikakati ya Tume ya Madini kwenye utoaji wa elimu kwa wananchi, Profesa Manya alieleza kuwa Tume ya Madini itaendelea kutumia vyombo vya habari, tovuti, mitandao ya kijamii na majukwaa mbalimbali katika kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo kwenye Sekta ya Madini.