THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINING COMMISSION

WANUFAIKA WA UCHIMBAJI MDOGO WA MADINI WAISHUKURU SERIKALI


news title here
21
Oct
2021

Kutokana na soko la dhahabu kuwa juu, wachimbaji wadogo wa Madini ya dhahabu waliopo Mkoa Morogoro wamenufaika na shughuli za Uchimbaji kwani hujipatia kipato na kukidhi mahitaji yao.

Hayo yamebainishwa tarehe 13.10.2021 na Wachimbaji wadogo wa Mgodi wa dhahabu wa Yakub Bishagazi Ngimbwa (YBN Gold Mine) uliopo katika kitongoji cha Mazizi, Kijiji cha Maseyu , Wilaya Morogoro walipotembelewa na Timu ya Wataalamu kutoka Tume ya Madini na Waandishi wa Habari wa Imaan Media Mkoani Morogoro kwa lengo la kutangaza fursa za Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini.

"Serikali kupitia Tume ya Madini imetoa mchango mkubwa baada ya kutupa elimu ya Uchimbaji na uchenjuaji uliotuongezea tija kwenye shughuli zetu za Uzalishaji", alisema mmiliki wa Mgodi Bw. Yakub Bishagazi.

Mmoja wa wafanyakazi wa Mgodi wa dhahabu wa Yakub Bishagazi Ngimbwa (YBN Gold Mine) Bw. Adam Yunus amesema usalama ndani ya mgodi ni mkubwa na hakujawai kutokea maafa yoyote toka Mgodi ulipoanza mwaka 2006.