THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINING COMMISSION

WAZIRI NA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MADINI WATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA MADINI KWENYE MAONESHO YA SABASABA


news title here
07
Jul
2021

Tarehe 05 Julai, 2021 Waziri wa Madini, Doto Biteko na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila wametembelea Banda la Wizara ya Madini katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya viongozi hao kutembelea banda Ia Wizara ya Madini na Taasisi zake pamoja na ya wadau wa madini, wamepongeza kasi ya utoaji wa elimu kwa wananchi wanaotembelea banda hilo kwenye maonesho.

Akielezea mafanikio ya Sektaya Madini kupitia mahojiano maalum na waandishi wa habari, Waziri Biteko ametaja kuwa ni pamoja na ongezeko la kasi ya utoaji wa leseni za madini kupitia uanzishwaji wa ofisi za maafisa madini wakazi wa mikoa, uanzishwaji wa masoko ya madini, kuimarika kwa udhibiti wa utoroshaji wa madini nchini, utoaji wa huduma kwa jamii na migodi ya madini, kuimarika kwa usimamizi wa mazingira na ushirikishwaji wa watanzania kwenye Sekta ya Madini.

Katika hatua nyingine, Bilionea wa Tanzanite Laizer Saniniu ametembelea na kushiriki katika maonesho ndani ya banda la Wizara ya Madini.