THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINING COMMISSION

WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA MADINI KWENYE MAONESHO YA SABASABA


news title here
05
Jul
2021

Tarehe 04 Julai, 2021 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula ametembelea banda la Wizara ya Madini na Taasisi zake katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

Mara baada ya kutembelea banda hilo ameipongeza Wizara ya Madini na Taasisi zake kwa maandalizi mazuri yaliyopelekea banda hilo kuwa kivutio kwa mamia ya wananchi wanaofurika katika banda hilo kupata elimu na huduma mbalimbali.

"Nimefurahi sana kuona banda hili likiwa na mvuto wa kipekee kwa kushirikisha wachimbaji wakubwa, wachimbaji wa kati, wachimbaji wadogo, masonara, soko la madini, watoa huduma kwenye migodi na hata wakina mama wakiwa na bidhaa nzuri zinazotokana na madini na kufanya maonesho kuwa ya kiwango cha kimataifa, amesema Mhe. Balozi Mulamula.