THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINING COMMISSION

News


 • news title here
  29
  Oct
  2019

  MWENYEKITI TUME YA MADINI AFANYA ZIARA DODOMA

  Leo tarehe 29 Oktoba, 2019 Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula amefanya ziara Wilayani Dodoma Mjini lengo likiwa ni kukagua shughuli za uchimbaji wa madini ya ujenzi pamoja na kutatua kero mbalimbali. Read More

 • news title here
  11
  Oct
  2019

  TUME YA MADINI YAENDESHA MAFUNZO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO WA BAJETI YA MWAKA 2019-2020 KWA WATENDAJI

  Tarehe 03 Oktoba, 2019 Kurugenzi ya Huduma za Tume ilitoa mafunzo ya namna ya utekelezaji wa mpango wa bajeti ya mwaka wa fedha 2019/2020 kwa watendaji jijini Dodoma lengo likiwa ni kuwajengea uwezo wa namna ya kusimamia matumizi ya fedha kwenye utekelezaji wa majukumu yao. Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyomalizika tarehe 05 Oktoba, 2019 yalishirikisha Wakurugenzi na Mameneja kutoka Makao Makuu ya Tume ya Madini,Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa, pamoja na maafisa bajeti. Read More

 • news title here
  11
  Oct
  2019

  TUME YA MADINI PAMOJA NA TAASISI ZA WIZARA YA MADINI YASHIRIKI MAONESHO YA SADC

  Tume ya Madini pamoja na Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini, ilishiriki katika maonesho ya kimataifa ikiwa ni sehemu ya mkutano wa 39 wa Wakuu wa SADCuliofanyika kuanzia tarehe 05 Agosti, 2019 hadi tarehe 09 Agosti, 2019 katika ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam. Read More

 • news title here
  10
  Oct
  2019

  WATUHUMIWA WIZI WA MADINI WAFIKISHWA MAHAKAMANI

  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imewafikisha Mahakamani Watuhumiwa Wanane (8) kwa makosa mbalimbali likiwemo la kuingia katika Mgodi wa North Mara na kuiba mifuko 15 ya Mawe yenye Dhahabu yanayokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 234 za kitanzania. Read More

 • news title here
  10
  Oct
  2019

  TUME YA MADINI, MKOMBOZI SEKTA YA MADINI

  Ili kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi, Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli ilitenganishailiyokuwa Wizara ya Nishati na Madini na kupelekea kuanzishwa kwaWizara ya Madini. Read More

 • news title here
  10
  Oct
  2019

  TUME YA MADINI YATWAA UBINGWA KWENYE MAONESHO YA SABASABA

  Tume ya Madini imefanikiwa kupata kikombe cha ushindi kwenye Kundi la Nishati na Madini katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kikombe hicho kilikabidhiwakwenye sherehe za ufunguziwa maonesho hayo na Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Samia Suluhu Hassan Read More